Fursa
AI Diffusion Pathways for Agriculture (AIDPA) ni programu ya miezi sita inayoendeshwa na AI Hub for Sustainable Development (inayoongozwa kwa pamoja na Wizara ya Biashara na Made in Italy pamoja na Shirika la Maendeleo la Umoja wa Mataifa - UNDP), huku DeepLeaf ikiwa mshirika wa utekelezaji na jukwaa la kidijitali.
Sekta ya kilimo inakabiliwa na changamoto zinazoongezeka za mabadiliko ya tabianchi. Wakulima wanahitaji mwongozo unaozingatia sayansi na data ili kulinda mazao yao na kuhakikisha mashamba yao yanaendelea kuwa na tija kiuchumi, hata hivyo, maarifa hayo mara nyingi hayawafikii kwa wakati na mahali wanapoyahitaji. Matokeo yake, wakulima wanaendelea kufanya maamuzi wakiwa na ushauri mdogo au uliochelewa. Programu hii inashughulikia changamoto sugu: maarifa ya kilimo yapo kwa wingi, lakini mara nyingi hayawafikii wakulima wakati na mahali wanapoyahitaji.
Maendeleo katika akili mnemba (AI) na miundombinu ya kidijitali yanatoa njia ya kuziba pengo hili la maarifa na kuifanya teknolojia ya kilimo kuwa injini ya usalama wa chakula. Hata hivyo, makampuni yanayoleta uvumbuzi wa AI kwa wakulima yanahitaji mtaji, uwezo wa kiufundi, ushirikiano, na data za kuaminika za ndani ili kujenga huduma zinazotegemeka.
AIDPA husaidia makampuni haya kushinda vikwazo hivyo na kuendeleza huduma zinazokidhi mahitaji ya kilimo ya ndani, zinazopatikana kwa urahisi kwa wakulima, na zinazozingatia mifumo endelevu ya kibiashara. Kwa kuunganisha teknolojia kutoka nchi za G7 na maarifa yaliyothibitishwa ya ndani, AIDPA huwezesha makampuni kujenga suluhisho za AI zinazofaa kwa masoko yao.
Wakati huo huo, programu hii huandika uzoefu wa kila kampuni ili kuonyesha ni uwezo, mbinu, na ushirikiano upi unaoweza kutumika tena na upi unaohitaji kurekebishwa kulingana na mazingira ya ndani. Masomo haya yatachangia katika azma ya AI Hub na washirika wake ya kuunda Njia 100 za Usambazaji wa AI (AI Diffusion Pathways) ifikapo mwaka 2030.
2. Fursa za uwekezaji
Kutoka sifuri hadi moja ndani ya miezi sita: kuanzia ujenzi wa kiufundi hadi matumizi
AIDPA inachukulia AI kama miundombinu ya pamoja, hivyo biashara hazihitaji kutumia rasilimali chache kujenga teknolojia kuanzia mwanzo. Badala yake, zinaweza kujikita katika kuifanya AI ifanye kazi kulingana na uhalisia wa maeneo yao na kujenga biashara zinazoleta uvumbuzi kwa wakulima.
Biashara zilizochaguliwa hupata teknolojia bila malipo, mafunzo na maarifa ya kuikabiliana na changamoto za kilimo za maeneo husika, pamoja na kuunganishwa na wateja watarajiwa ili biashara zao ziweze kustawi na kudumu. Kufikia mwisho wa programu, kila biashara inatarajiwa kuwa na bidhaa iliyokamilika kulingana na mahitaji ya eneo husika na iliyojaribiwa na watumiaji halisi, pamoja na uwezo wa kuendeleza huduma zake baada ya programu kumalizika.
Hasa zaidi, programu hii inajumuisha:
01

Upatikanaji wa Mfumo
Upatikanaji wa mfumo wa AI, vifaa vya ukuzaji programu (SDKs) na violesura vya programu (APIs) bila malipo hadi tarehe 31 Julai 2027.
02

Warsha za kikundi
Vikao vya vitendo kwa kundi zima kuhusu teknolojia, ukuzaji wa bidhaa, na kuwafikia wateja.
03

Warsha za uwekezaji
Vikao vilivyobuniwa kulingana na mahitaji ya kiufundi, kibiashara, na soko la ndani ya kila mradi.
04

Tathmini za kiufundi
Usaidizi wa kujenga, kuunganisha na kurekebisha bidhaa ya mradi.
05

Ukaguzi wa maendeleo
Tathmini za mara kwa mara ili kubaini changamoto na kuelekeza hatua zinazofuata.
06

Majaribio na utekelezaji
Upatikanaji wa maeneo ya majaribio, watumiaji halisi na utambulisho kwa wateja, kwa kuungwa mkono na washirika wa ndani na maarifa ya kilimo yaliyothibitishwa.
Matokeo yanayotarajiwa
Biashara zinabaki na umiliki wa bidhaa zao, uhusiano na wateja, mifumo ya kidijitali, data za uendeshaji wa ndani, na mifano ya biashara, kwa kuzingatia mikataba na sheria husika. Uwezo wa kuhamisha huduma ni kanuni muhimu ya programu hii, inayowezesha biashara kuendeleza huduma zao baada ya kipindi cha ushirikiano bila kufungwa na mtoa huduma mmoja pekee.
Nani anaweza kuomba
Mpango huu kwa sasa unapatikana katika nchi saba za majaribio: Ghana, Italia, Kenya, Morocco, Rwanda, Tanzania na Tunisia. Mradi mmoja utachaguliwa katika kila nchi. Waombaji lazima wawe na makazi, waendeshe shughuli zao, au waonyeshe nia ya dhati ya kufanya kazi katika mojawapo ya nchi hizi.
Mpango huu uko wazi kwa miradi ya teknolojia ya kilimo katika hatua yoyote, kuanzia wazo la awali hadi suluhisho lililoendelezwa zaidi. Waombaji wanaostahiki ni pamoja na kampuni changa, biashara za kijamii, na mashirika mengine yanayounda huduma zinazotumia akili mnemba (AI) kwa ajili ya kilimo. Waombaji binafsi wanaweza pia kustahiki ikiwa watawasilisha mpango wenye mvuto. Bila kujali hatua waliyopo, waombaji watakaochaguliwa watapata fursa ya kutumia teknolojia ya AI, mwongozo wa wataalamu, na ushirikiano muhimu ili kujenga au kukuza uvumbuzi wao.
Vigezo vya uteuzi vinajumuisha uwezo wa waombaji kutekeleza mipango yao, umuhimu wa huduma inayopendekezwa kwa vipaumbele vya maendeleo ya ndani, upatikanaji wa maarifa ya kilimo ya eneo husika, utayari wa bidhaa, matumizi ya uwajibikaji ya data, na uendelevu wa kibiashara. Tunatafuta timu zenye tatizo la kilimo linaloeleweka, uhusiano wa kuaminika au njia ya kuwafikia wakulima, na nia ya kujenga na kujaribu huduma ndani ya miezi sita.